Umoja wa Mataifa:Ukatili unaendelea DRC:
11 Novemba 2003Matangazo
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, inajionea mauaji makubwa ya kiholela na vitendo vya jinai dhidi ya utu kiasi ambacho ni miongoni mwa nchi zinazokanyaga haki za Binaadamu duniani. Mtayarishaji wa ripoti maalumu ya Umoja wa Mataifa kuhusu DRC, Bibi Iulia Motoc, amesema kuwa vitendo vya kikatili na vya kutisha vinavyoendelea katika nchi hiyo ya Kiafrika, ambako Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakishambuliwa, vinaweza vikasababisha uchunguzi wa kimataifa ufanywe. Bibi Motoc amesema kuwa uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu katika Kongo-Kinshasa ni vitendo vya jinai vya kimataifa ambavyo vinakwenda kinyume kabisa na ulinzi wa binaadamu wote. Ripoti yake inasema kuwa mauaji ya kiholela, vitendo vya jinai dhidi ya utu na vitendo dhidi ya uadilifu wa vita ni mambo ya kawaida nchini humo licha ya kufikiwa mapatano ya amani mwezi wa Aprili mwaka huu.