1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kufanya mazungumzo na nchi za Balkan

18 Desemba 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa leo kufanya mazungumzo na wenzao kutoka nchi za eneo la Balkan Magharibi mjini Brussels juu ya kuimarisha uhusiano kati yao.

https://p.dw.com/p/4oI4i
Belgien Brüssel 2024 | EU-Außenminister beraten über Ukraine-Konflikt und Nahost-Situation
Picha: FREDERIC SIERAKOWSKI/European Union

Nchi sita za Balkan Magharibi – Albania, Bosnia-Herzegovina, Kosovo, Montenegro, Macedonia Kaskazini na Serbia – zote zimeonyesha nia ya kujiunga na Umoja wa Ulaya na zimekuwa zikisubiri kwa muda mrefu kufanya hivyo.

Hata hivyo Umoja wa Ulaya haujaonyesha nia ya kuharakisha mchakato wa kuziruhusu nchi hizo kujiunga na Umoja huo japo mageuzi yanayohitajika kuelekea huko yameanza kushika kasi katika baadhi ya nchi hizo za Balkan Magharibi.

Umoja wa Ulaya unapania kutumia uhusiano mzuri kati yao na nchi za Balkan Magharibi kujaribu kukabiliana na ushawishi wa China na Urusi katika eneo hilo la Balkan.