1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na mageuzi ya sera ya wahamiaji

7 Aprili 2016

Umoja wa Ulaya umewasilisha mpango mpya utakaoifanyia mageuzi sera ya wahamiaji lakini mwandishi wa DW Brussels, Bernd Riegert, anasema mzozo wa wakimbizi hautatatuliwa na mapendekezo ya halmashauri ya Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/1IRHt
Deutschland Stempel Abgeschoben Symbolbild
Picha: Reuters/M. Dalder

Mapendekezo hayo yanataka kuangazia zaidi sheria ya kuomba hifadhi katika nchi za Umoja wa Ulaya, lakini ni kwa namna gani na lini mapendekezo hayo yatatekelezwa?

Nyaraka za siri za Halmashauri ya Ulaya zilizopatikana hivi karibuni kutoka kwa duru za Umoja wa Ulaya mjini Brussels, zimeeleza kuwa Halmashauri kuu ya umoja huo inataka kupendekeza kwa nchi wanachama kuushughulikia mchakato wa kuomba hifadhi.

Maamuzi kuhusu maombi ya hifadhi yatapitiwa na maafisa wa Ulaya, jambo ambalo linaonekana kama ni maendeleo zaidi katika sera ya wakimbizi. Makamu Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Frans Timmermans, alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa vipengele muhimu vya nyaraka za kuomba hifadhi vitaondolewa.

Timmermans na Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulika na uhamiaji, Dimitris Avramopoulos, wanaamini kuwa nchi wanachama hazitatumia haki ya uhuru wao katika kuamua maombi gani ya hifadhi yatakubaliwa na yapi hayatokubaliwa.

Muswada kuidhinishwa na Bunge la Ulaya

Pendekezo rasmi la mageuzi ya mfumo wa kuomba hifadhi, litawasilishwa tu baada ya mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi wanachama za Umoja wa Ulaya yatakayofanyika katika majira ya joto. Muswada huo kisha utahitajika kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri na Bunge la Ulaya.

Makamu Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Frans Timmermans
Makamu Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Frans TimmermansPicha: picture-alliance/dpa/L. Dubrule

Hata hivyo, kuna uchaguzi wa aina mbili uliopendekezwa, ambapo kama kile kinachoitwa makubaliano ya Dublin yataendelea kutumika na yanaweza tu kuondolewa kupitia utaratibu wa dharura. Kila nchi itakayokuwa ya kwanza kumpokea mhamiaji, ni wajibu wa nchi hiyo kushughulikia mchakato wa maombi ya hifadhi ya mhamiaji huyo.

Na uchaguzi wa pili itakuwa ni kuondoa makubaliano ya Dublin, vigezo vinaweza kubadilishwa kwa kuamua nchi gani wanachama zinahusika kwa maombi ya hifadhi.

Inaonyesha bila shaka Timmermans anapendelea zaidi uamuzi wa pili, kwa sababu anasema mfumo wa sasa makubaliano ya Dublin haufai. Amesema mfumo huo umeshindwa kuleta tija, hivyo kuna haja ya kuufanyia mageuzi. Pendekezo jipya linahusisha mchakato mmoja wa kuomba hifadhi na mahitaji ya maombi ya hifadhi katika nchi zote 28 wanachama.

Markus Ferber, mwakilishi wa chama cha CSU, anayehusika na sera za uhamiaji kwenye Umoja wa Ulaya, ameiambia DW kwamba pendekezo kama hilo lililowasilishwa na halmshauri ya umoja huo, limemshangaza. Anasema angefikiria kidogo lingekuwa la kijasiri katika utawala mkubwa kama huo ili kuweza kufanikiwa katika hadhi ya Ulaya.

Mwandishi: Bernd Riegert
Tafsiri: Grace Patricia Kabogo/DW http://bit.ly/23dZtxo
Mhariri: Iddi Ssessanga