1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN, Iran zahimiza ushirikiano kukabili dhoruba za mchanga

9 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa na Iran zimesema leo kuwa mataifa katika Mashariki ya Kati, Afrika na Asia lazima yashirikiane kukabiliana na dhoruba za mchanga na vumbi zinazozidi kuwa kali kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

https://p.dw.com/p/4W96Q
Dhoruba ya mchanga
Dhoruba ya mchangaPicha: W. G. Allgoewer/blickwinkel/picture alliance

Katika hotuba kwa njia ya video kwa wawakilishi wa takriban mataifa 50 na mashirika 15 yanayohudhuria kongamano la kimataifa la kukabiliana na dhoruba za mchanga na vumbi nchini Iran, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amewahimiza washirika wa kongamano hilo kutumia muda wao mjini Tehran kujenga uhusiano, kuimarisha ushirikiano na kujitolea kwa hatua zinazoweza kutekelezwa.

Soma zaidi: Iraq yakumbwa tena na dhoruba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa

Wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, rais wa Iran Ebrahim Raisi, alitoa wito kwa mataifa katika kanda hiyo kuanzisha mfuko wa kutafuta suluhu za pamoja, na amezilaumu nchi zilizoendelea kiviwanda kwa kusababisha matatizo mengi, kupuuzia masuala ya mazingira.

Kulingana na wataalamu wa hali ya hewa, dhoruba za mchanga na vumbi zinatarajiwa kuongezeka katika nchi zinazokabiliwa na hatari zaidi ya mabadiliko ya tabianchi.