UN: Mazungumzo ya bayoanuwai COP16 kuanza tena Februari
28 Novemba 2024Matangazo
Mkutano huo wa bayoanuwai utafanyika katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo - FAO kuanzia Februari 25 hadi 27 ili kushughulikia masuala "yaliyoachwa bila kutatuliwa kufuatia kusimamishwa kwa mkutano huo" mnamo Novemba 2.
Kongamano la ulinzi wa mazingira COP16 laanza Colombia
Washiriki 23,000 walimiminika mjini Cali nchini Colombia kwa mkutano mkubwa zaidi wa kilele kuhusu bayoanuwai uliolenga kulinda mazingiraasili dhidi ya ukataji miti, mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira.
Mazungumzo yaliingia hadi usiku wa ziada lakini Colombia ambayo ndio ilishika uwenyekiti wa mkutano huo ikashindwa kupata idadi ya kutosha ya washiriki, baada ya wengi kuondoka mapema kurudi makwao.