1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhuru wa vyombo vya habari

Waandishi 250 wamekamatwa tangu Taliban waingie madarakani

26 Novemba 2024

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Afghanistan leo Jumanne umesema utawala wa Taliban umewakamata kiholela na kuwazuia wanahabari 256 tangu ulipochukua madaraka miaka mitatu iliyopita.

https://p.dw.com/p/4nQm7
Klabu ya waandishi wa habari ya Peshawar Pakistan
Klabu ya waandishi wa habari ya Peshawar PakistanPicha: Faridullah Khan/DW

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Afghanistan leo Jumanne umesema utawala wa Taliban umewakamata kiholela na kuwazuia wanahabari 256 tangu ulipochukua madaraka miaka mitatu iliyopita.

Katika ripoti hiyo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Roza Otunbayeva, amesema waandishi wa habari nchini Afghanstan mara nyingi wanakabiliwa na sheria zisizo wazi juu ya kile wanachoweza kuripoti.Waandishi Habari wa DW waondolewa Afghanistan

Katika jibu lililoambatana na ripoti hiyo, wizara ya mambo ya kigeni inayoongozwa na Taliban imekanusha madai hayo na kusema kwamba watu iliyowakamata ni  wahalifu.

Aidha wizara hiyo imedai kwamba ripoti hiyo haina ukweli wowote na kwamba vikosi vya usalama vinafanya kazi kuwalinda waandishi wa habari.