1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF Migogoro imewafanya watoto wateseka zaidi hivi sasa

28 Desemba 2024

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema kuna idadi kubwa ya watoto wanaishi katika maeneo ya migogoro au wamelazimishwa kuyahama makaazi yao kutokana na migogoro hiyo.

https://p.dw.com/p/4odsU
UNICEF Impfkampagne für Kinder im Sudan
Mtoto wa Sudan chanjo wakati wa kampeni ya kukabiliana na janga la polio na kutokomeza upungufu wa vitamini A, Juni 9, 2024. Picha: Ebrahim Hamid/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo iliyotolewa leo hii, watoto milioni 473 wanakadiriwa kuishi katika maeneo yenye migogoro ikiwa ni makadirio ya zaidi ya mtoto mmoja kati ya sita duniani kote.Rekodi hizo zinamaanisha idadi ya watoto wanaoishi katika maeneo yenye migogoro imeongezeka mara mbili kutoka takribani asilimia 10 katika miaka 1990 hadi karibu asilimia 19 kwa wakati huu. UNICEF inasema pamoja na madhila mengine,watotohao wanauawa na kujeruhiwa, wanasitisha masomo, wanakosa chanjo muhimu au wanakabiliwa na utapiamlo mkali. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto milioni 47.2 waliyakimbia makaazi yao kutokana na migogoro na vurugu hadi mwishoni mwa 2023. Hali inaonesha katika mwaka huu unaomalizika wa 2024, kumekuwa na ongezeko kubwa kwa sababu ya migogoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Haiti, Lebanon, Myanmar, na Palestina na Sudan.