1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNITED NATIONS :Vikosi vya UN kuongezewa muda mpakani Ethiopia/Eritrea

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdT

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa linatangaza kuwa mzozo wa mpaka kati ya mnchi za Ethiopia na Eritrea ambao haujatatuliwa unasababisha matattizo kwenye eneo hilo.

Baraza hilo linatoa wito kwa mataifa hayo mawili kuondoa vikosi vyao kwenye eneo la mpakani na kuidhinisha bila vikwazo kuongeza muda wa ujumbe wake kusimamia eneo hilo kwa miezi sita zaidi.Nchi ya Ethiopia ilipata uhuru wake mwaka 93 kufuatia vita vya msituni vilivyodumu miaka 30 huku eneo la mpakani likiachwa bila usimamizi rasmi.