1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

160409 Indien Wahlen

Charo Josephat16 Aprili 2009

Watu 11 wauwawa na waasi wa Mao

https://p.dw.com/p/HY1A
Waziri mkuu wa India Manmohan SinghPicha: AP Photo

Wapigaji kura zaidi ya milioni 700 kati ya raia bilioni 1.1 wa India wanatarajiwa hii leo kujitokeza vituoni kupiga kura katika uchaguzi mkubwa wa kidemokrasia duniani. Zoezi hilo litakaloedelea kwa mwezi mmoja, halitarajiwi kutoa mshindi wa moja kwa moja kuiongoza nchi hiyo huku ikikabiliana na mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Mauaji yatokea

Watu takriban 11 wameuwawa mapema leo na waasi wa Mao mashariki mwa India. Katika jimbo la Jharkhand, waasi wa Mao wamelipua bomu la kutegwa ardhini na kulishambulia basi lililokuwa limewabeba maafisa wa usalama waliokuwa wakienda kushika doria katika vituo vya kupigia kura. Wanajeshi tisa na raia wawili wameuwawa katika hujuma hiyo iliyotokea takriban kilomita 140 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo, Ranchi.

Katika mkoa jirani wa Bihar, maafisa wawili wa usalama wamepigwa risasi na kuuwawa na waasi wa wilaya ya Gaya. Milio ya risasi imesikika katika wilaya ya Bijapur na Dantewada, sehemu ya eneo la msitu lililo ngome ya waasi wa mrengo wa kushoto.

Chochote chaweza kutokea

Uchaguzi wa India uko wazi kabisa. Hata waangalizi hawajawahi hata mara moja kutoa maoni kuhusu nani atakayeshinda uchaguzi huo. Lakini kuna mengi ambayo ni bayana. Sonia Ghandi, kiongozi wa chama tawala cha Congress atakabidhi kazi ya kuongoza shughuli za serikali mikononi mwa waziri mkuu wa sasa Manmohan Singh iwapo chama cha Congress kitashinda uchaguzi huo.

Bila mbari ya Gandhi-Nehru nchini India, siasa za nchi hiyo tangu ilipojipatia uhuru zimedhihirsha wazi dhahiri shahiri kwamba chama cha Congress kingekuwa katika nafasi mbaya, anasema mchambuzi wa kisiasa nchini India, Narasimha Rao.

"Familia ya Gandhi ina ushawishi mkubwa kwa hiyo bila shaka chama cha Congress bila msaada wa jina la familia hiyo, kingekuwa kibaya zaidi kuliko kilivyo leo. Watu huzitegemea familia za aina hii kuyashughulikia masilahi yao, kwa hiyo familia hizi huwapa kiwango fulani cha matumaini."

Mtoto wa kiume wa Sonia Ghandi, Rahul, tayari ni mwanafamle atakayerithi utawala wa chama cha Congress. Yeye ni wa kizazi cha tano cha ukoo wa Gandhi.

Katika kampeni za uchaguzi, chama cha Congress awali ya yote kimepigia debe ufanisi wa sera zake za uchumi na kijamii. Kimetumia ukuaji imara wa uchumi unaofikia hadi asilimia 9 na kuchipuka kwa viwanda, uhusiano mzuri wa karibu na Marekani na bidii ya kuendeleza mdahalo na nchi jirani ya Pakistan.

Chama cha upinzani cha BJP kinailumu serikali kwa matatizo katika utekelazaji wa mipango ya misaada na kinaielekezea kidole cha lawama kwa kuzembea usalama wa ndani na vita dhidi ya ugaidi. Kufuatia mashambulio dhidi ya mji wa Mumbai, mgombea wa wadhifa wa waziri mkuu wa chama cha Baharatiya Janati, BJP, L K Advani mwenye umri wa miaka 81, anasema mashambulio hayo yalipangwa nchini Pakistan, matamshi ambayo yanakubaliwa na wapigaji kura wengi nchini India.

"Kidole cha la tuhuma kinaelekezwa, bila kukosea, kwa jirani wetu Pakistan. Kuhojiwa kwa gaidi aliyekamatwa kumefichua ushahidi muhimu. Nchi walikotokea magaidi 10 walioishambulia India imejulikana. Pia kuna ushahidi mwingi uliokusanywa kwenye chombo cha kuvulia samaki na maiti za magaidi ambao umewasaidia wachunguzi kutathmini mfululizo wa matukio kutoka yalikoanzia hadi yalikofanywa."

L.K. Advani
Mgombea wa chama cha BJP L.K.AdvaniPicha: UNI

Hakutakuwa na mshindi wa wazi

Miongoni mwa vyama vikubwa vya kisiasa hakuna kinachotarajiwa kupata ushindi wa moja kwa moja wa kura. Mkwamo kati ya chama cha Congress na chama cha BJP, unaweza kuvinufaisha vyama vya kikomunisti na kimkoa, hata ikiwa havina mpango wa pamoja.

Kiongozi wa chama cha Bahujan Samaj, Mayati Kumari, ambaye pia ni waziri mkuu mwenye ushawishi mkubwa wa jimbo kubwa la India la Uttar Pradesh, anaweza kupata idadi kubwa ya kura za watu wa tabaka la chini nchini humo, kwa hujitokeza kwa wingi kuopiga kura ikilingainishwa na Wahindi wa tabaka la kati. Huyu hapa Narasimha mchambuzi wa kisiasa wa India.

"Kushiriki na shauku ya kubadili mkondo wa mambo ina nguvu miongoni mwa watu wa tabaka la chini."

Bila shaka rushwa, upendeleo wa ndugu katika utajiri, utendaji mbaya wa kazi wa idara za serikali na vyombo vya usalama safari hii vimelichochea tabaka la kati. Wakati kura zitakapohesababiwa mwezi Mei na matokeo ya viti vya bunge yatakapojulikana, kutaanza mazungumzo ya kuunda serikali mpya ya India.

Kwa sababu za kiratibu na kiusalama kutakuwa na siku tano za uchaguzi, siku ya mwisho ikiwa Mei 13. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa Mei 16.

Mwandishi: Matthay, Sabina/Charo Josephat

Mhariri: Aboubakar Liongo