1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wataka matokeo ya uchaguzi wa rais DRC yafutwe

Abdu Said Mtullya30 Novemba 2011

Kura zinaendelea kuhesabiwa huko DRC baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu hapo juzi, huku waangalizi wa uchaguzi huo wakitoa taarifa juu ya kuwepo udanyanyifu na vurumai katika sehemu nyingi.

https://p.dw.com/p/13JJ0
Mpigakura wa upinzani akilalamikia wizi wa kura kwenye uchaguzi wa DRC.
Mpigakura wa upinzani akilalamikia wizi wa kura kwenye uchaguzi wa DRC.Picha: dapd

Wagombea wanne wa upande wa upinzani wanaompa Rais Joseph Kabila changamoto wametoa mwito wa kuyabatilisha matokeo ya uchaguzi wakidai kwamba umefanyika udanganyifu mtindo mmoja.

Lakini wachunguzi wanahofia huenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ikarudia tena katika mgogoro ikiwa matokeo ya uchaguzi hayatakubaliwa.

Uchaguzi huo ulioanza Jumatatu, ni wa pili kufanyika tokea kumalizika kwa vita nchini Kongo na ni wa kwanza kuandaliwa na serikali ya nchi hiyo ,badala ya jumuiya ya kimataifa.

Rais Joseph Kabila anaewania muhula mwingine anatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo ,kutokana na wapinzani kugawanyika.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa tarehe 6 Disemba.