Urusi imedai kuyazuia mashambulizi ya droni kutoka Ukraine
21 Agosti 2023Matangazo
Moscow,
Urusi imesema imezuia mashambulio mawili ya droni kutoka Ukraine katika eneo la mji wa Moscow na hakuna kifo chochote kilichoripotiwa.Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Urusi imesema jaribio la Ukraine la kutaka kushambulia kwa ndege zisizoendeshwa na rubani limezuiwa majira ya alfajiri. Kwa mujibu wa Urusi, droni hizo zimezuiwa kupitia kile ilichokiita mifumo maalum ya kieletroniki ya kivita, na kuangukia katika kijiji cha Pokrovskoye kusini magharibi mwa mji mkuu, Moscow. Shirika la habari la RIA Novosti limesema safari za ndege kutoka viwanja viwili vya ndege vya kimataifa kwenye eneo hilo zilisimama kwa muda na ndege kuelekezwa kutuwa katika maeneo mengine.