Urusi: Ukraine imekuwa ikitumia silaha za kemikali
18 Desemba 2024Matangazo
Msemaji wa wizara hiyo Maria Zakharova amesema wana ushahidi juu ya matumizi ya kemikali hiyo ya sumu iliyotumiwa na Ukraine, japo hakutoa maelezo ya kina kuhusu ushahidi huo.
Hata hivyo, hakukuwa na tamko kutoka upande wa Ukraine ambayo nayo imeituhumu Urusi kwa kutumia kemikali hiyo ya sumu.
Wakati huo huo, Urusi imesema itajibu vikwazo iliyowekewa na Umoja wa Ulaya ambavyo Moscow inavichukulia kuwa hatari kwa usalama wa nishati duniani.