SiasaUrusi
Urusi yaadhimisha kuyanyakua majimbo ya Ukraine kwa tamasha
29 Septemba 2023Matangazo
Kumbukumbu hiyo inaambatana na tamasha litakalofanyika katika uwanja wa kihistoria wa Red Square, mjini Moscow, ambalo linalenga kuutambulisha umma likizo mpya itakayokuwa ikiadhimishwa nchini humo.
Hata hivyo, vikosi vya Urusi havidhibiti kikamilifu majimbo ya Kherson, Zaporizhzhia, Donetsk na Luhansk, na imelazimika wakati mwingine kusalimisha maeneo kadhaa kufuatia mashambulizi ya Ukraine.
Wakati huo huo, makabiliano baina ya Urusi na Ukraine yameendelea kuripotiwa sehemu mbalimbali. Idara ya ulinzi wa anga ya Moscow imesema imeziharibu ndege 11 zisizo na rubani zilizorushwa na Ukraine katika maeneo ya Kursk na katika mkoa wa Kaluga takriban kilomita 200 kusini-magharibi mwa Moscow.