Urusi yadungua droni iliokuwa inakaribia mji wa Moscow
31 Agosti 2023Hayo yameelezwa na meya wa Moscow Sergei Sobyanin kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wa mtandao wa Telegram leo Alhamisi.
Amesema wanajeshi wa ulinzi wa angakatika wilaya ya Voskresensky iliyoko takriban kilomita 60 kutoka Moscow waliiharibu droni hiyo iliyokuwa ikielekea Moscow, japo hakusema wapi ilikotokea.
Soma pia:Mashambulizi ya droni ya Ukraine dhidi ya Moscow yanaweza kuongezeka
Hata hivyo baadae wizara ya ulinzi ya Urusi ilitowa taarifa ikisema ndege hiyo ilikuwa ya Ukraine.
Hakuna kifo wala uharibifu uliosababishwa na tukio hilo kwa mujibu wa meya na watoa huduma za dharura wapo katika eneo la tukio.
Jana maeneo mengi ya Urusi yalilengwa na mashambulizi makubwa ya Usiku ikiwemo uwanja wa ndege wa Pskov ulioko karibu na mpaka wa Estonia.