1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaipata miili ya watu 10 na vinasa sauti vya ajali

Sylvia Mwehozi
26 Agosti 2023

Mamlaka za Urusi zimetangaza kuipata miili ya watu 10 katika eneo la ajali ya ndege inayodhaniwa kumuua mkuu wa kundi la mamluki la Wagner,Yevgeny Prigozhin.

https://p.dw.com/p/4VbI5
Russland | Jewgeni Prigoschin | mutmaßliches Flugzeugunglück in der Region Twer
Picha: Investigative Committee of Russia/Handout/REUTERS

Mamlaka za Urusi zimetangaza kuipata miili ya watu 10 katika eneo la ajali ya ndege inayodhaniwa kumuua mkuu wa kundi la mamluki la Wagner,Yevgeny Prigozhin.

Kamati inayochungaza ajali hiyo, imesema katika taarifa yake kupitia mtandao wa Telegram kwamba imefanikiwa pia kuvipata vinasa sauti.

Nchi kadhaa za Magharibi zimependekeza kuwa huenda Moscow ndiyo iliyohusika na ajali hiyo, kwa kuzingatia kwamba imetokea miezi miwili tu baada ya uasi wa muda mfupi wa Prigozhin dhidi ya jeshi la Urusi.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi ya Kremlin Dmitry Peskov alikanusha vikali siku ya Ijumaa madai ya kuhusika kwa Moscow, akielezea uvumi unaozunguka ajali hiyo kama uongo mtupu.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kwamba tathmini ya awali ya shirika la ujasusi la Marekani imehitimisha kuwa ndege hiyo ilidunguliwa na mlipuko wa kukusudia.