Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni 12 na kombora
3 Desemba 2023Mashambulizi hayo yameripotiwa na jeshi la anga la Ukraine leo asubuhi lakini hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na Moscow.
Ripoti ya jeshi hilo la Ukraine imesema droni zilizorushwa aina ya Shahed zinazotengenezwa nchini Iran, zilikuwa zimeelekezwa Kaskazini Magharibi mwa Ukraine na lakini nyingi ziliangushwa katika eneo la Mykolaiv Kusini mwa Ukraine.
Soma pia:Urusi yaendeleza mashambulizi mashariki mwa Ukraine
Hakukuwa na ripoti za haraka kuhusu uharibifu uliotokana na kuangushwa kwa ndege hizo na nyingine mbili ambazo hazikuharibiwa.
Kuhusu kombora hilo la masafa marefu lililorushwa na Urusi, Ukraine imesema halikuangushwa lakini pia halikufikia shabaha iliyokusudiwa.
Hata hivyo, ripoti ya jeshi hilo haikuweza kuthibitishwa kwa njia huru na pia hakukuwa na tamko la haraka kutoka Urusi.