Urusi yaushambulia uwanja wa ndege wa jeshi la Ukraine
27 Julai 2023Msemaji wa kikosi cha jeshi la anga cha Ukraine, Yuri Ihnat, amesema mashambulizi hayo yalizilenga ndege za kivita chapa Su-24 katika uwanja wa ndege wa Starokostyantyniv.
Ihnat amesema makombora mengine ya Urusi yalizuiwa kwenye miji ya Kiev, Kharkiv na Dnipro.
Jeshi hilo limesema jumla ya makombora 36 yalizuiwa jana jioni.
Soma zaidi: Urusi yaituhumu Ukraine kufanya mashambulizi ya droni Moscow
Kambi ya jeshi la anga ya Starokostyantyniv imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na jeshi la Urusi, tangu nchi hiyo ilipoivamia Ukraine.
Wakati huo huo, Jumuia ya Kujihami ya NATO imesema itaimarisha ulinzi katika eneo la Bahari Nyeusi.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Urusi kujiondoa kwenye makubaliano ambayo yaliruhusu meli zinazosafirisha nafaka ya Ukraine kupita kwa usalama kwenye bahari hiyo.