1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama barabarani

5 Septemba 2012

Kila siku ajali nyingi za barabarani ambazo zingeweza kuzuilika hutokea barani Afrika. Mchezo wetu wa redio unaonyesha jinsi ya kuwa salama barabani ukiwa mtembea kwa miguu, kwenye baisikeli, gari au lori.

https://p.dw.com/p/163vy
Learning by Ear – Road safety Fotograf | Bildagentur: © Andre Schumacher / LAIF (Drei Frauen auf Motorrad, Straße, Verkehr) ACHTUNG!! DIE DEUTSCHE WELLE HAT DIE NUTZUNGSRECHTE NUR BIS 1.9.2013!! EINSTELLUNGSDATUM: 09.09.2011
Learning by Ear - Road safetyPicha: LAIF

Makosa madogo yanaweza kusababisha ajali kubwa. Ajali hizo hutokea kwa sababu madereva wa mabasi/dala dala/matatu hawaangalii kulia kabla ya kuovertake, kwa sababu madereva wa malori huendesha katika maeneo ya vijijini kwa kasi kubwa na kwa sababu watoto hucheza barabarani bila kusimamiwa. Ajali hizi zinazotokea, zingeweza kuwa na madhara madogo zaidi kama abiria wangekuwa wanafunga mikanda au kama mabasi yasingekuwa yanajazwa kama ilivyo kawaida.

Nchini Angola, ugonjwa wa Malaria ndio chanzo kikuu cha vifo kwa vijana lakini chanzo kinachofuatia katika kusababisha vifo vya vijana wengi ni ajali za barabarani. Wakati huo huo, idadi ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani barani Ulaya imepungua kutokana na elimu juu ya kutumia mikanda pamoja na mbinu nyingine za kuepuhs ajali. Leo hii vifo vichache vinasababishwa na ajali za barabarani nchini Ujerumani ikilinganishwa na miaka ya 1950 ingawa sasa idadi ya magari imeongezeka. 

Katika mchezo huu wa redio tutafuatilia maisha ya familia ya Wanjiru na kusikia jinsi wanavyopata kuelewa jinsi ambavyo barabara za Afrika zinaweza kuwa hatari na wakati mwingine kusababisha maafa. Kisha tutazungumza na mtaalamu wa usalama barabarani Gilbert, kufahamu jinsi ya kuufanya usafiri barabarani kuwa salama zaidi na hivyo kuokoa maisha ya watu.

Vipindi vya Deutsche Welle “Learning by Ear – Noa Bongo! Jenga Maisha Yako” vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharic.