Hii leo Urusi imetangaza kwamba itaanzisha ushirikiano na China katika luteka za kijeshi wakati mvutano kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi ukiendelea kufukuta. Saumu Njama alizungumza na mchambuzi wa siasa za kimataifa Ahmed Rajab na kwanza alimuuliza hatua ya Urusi kuanzisha ushirikiano na China na Iran inatoa ujumbe gani kwa mataifa ya Magharibi?