Utambuzi wa kimataifa kwa mashujaa wa kwetu
31 Julai 2015Siku ya mwisho ya kuwasilisha simulizi imepita, lakini mashujaa wa kwetu bado wanasonga mbele. Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita tumepokea simulizi kuhusu mashujaa kutoka kila kona ya dunia. Visa hivi vimetusaidia kupata picha ya watu wanaoleta mabadiliko katika jamii zao. Ahsante kwenu nyote mliochangia kwa kuwasilisha simulizi zenu. Tutapitia ripoti zote zilizotufikia na katika wiki chache zijazo tutachagua mshindi. Unaweza kutazama vipindi vya televisheni vya DW kugundua mashujaa wengine wa kwetu na watu wanaosaidia kuleta mabadiliko duniani.
Orodha ya visa vya DW vya mashujaa wa kwetu
DW ni ya mashujaa wa kwetu. Watu wanaotegemea ufahamu wa kimataifa na wanaofikiri, kutafakari, kutafakari upya na kuvumbua mambo mapya. Watu wanaotengeneza sheria badala ya kuzifuata na wanaotia motisha wengine badala ya kuwa kikwazo. Tuko kwa ajili yao. Ni kazi yetu kuwaletea habari na taarifa wanazozihitaji kujenga dunia yao.
Mengi zaidi juu ya visa vingine vya mashujaa wa kwetu na matangazo mapya ya utapata kwenye ukurasa huu.
Zawadi
- Mshindi: Simu ya kisasa (Smartphone) na kifurushi cha shujaa wa mtaani
- Nafasi ya pili na ya tatu: iPod na kifurushi cha shujaa wa mtaani
- Zawadi ya kufutia machozi: Moja kati ya vifurushi saba vya shujaa wa mtaani