1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini yaendelea uchunguzi dhidi ya Rais Yoon

17 Desemba 2024

Korea Kusini imefanya jaribio jipya la kuvamia ofisi ya rais ili kupekua na kutafuta ushahidi katika uchunguzi unaotakiwa kubainisha uhalali wa jaribio la muda mfupi la Rais Yoon Suk Yeol la kutangaza sheria ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4oEcl
Südkorea, Seoul | Chu Mi-ae fordert gründliche Untersuchung der Rebellionsvorwürfe
Kamati ya Uchunguzi wa Uasi wa Chama cha Yoon Suk-yeol, pamoja na wabunge wapatao 20 wa kamati hiyo, huko Yongsan-gu, Seoul, Korea Kusini, Desemba 16, 2024Picha: Chris Jung/NurPhoto/picture alliance

Jopo la wachunguzi ikiwa ni pamoja na polisi na maafisa wa idara inayofuatilia vitendo vya rushwa kwa viongozi wakuu serikali limejaribu kukagua kompyuta za maafisa wa usalama wa rais ili kukusanya rekodi muhimu.Wakati huohuo, waendesha mashtaka wamemtaka Rais Yoon aliyeondolewa madarakani na bunge siku ya Jumamosi ajitokeze kuhojiwa au akabiliwe na uwezekano wa kukamatwa. Yoon, ambaye anasubiri uamuzi wa Mahakama ya Katiba kujua hatma yake, anachunguzwa kwa makosa ya kufanya uasi dhidi ya dola kutokana na kutangaza kwake sheria ya kijeshi mapema mwezi huu.