Rais wa Marekani Donald Trump amemteua Jaji Mhafidhina wa jimbo la Indiana Amy Coney Barrett kuchukua nafasi ya hayati Ruth Bader Ginsburg katika mahakama kuu. Hata hivyo, uteuzi wake umetiliwa mashaka na Wademocrat wanaosema mshindi wa urais wa Novemba 3 ndiye anapaswa kufanya uteuzi huo. Mchambuzi wa siasa Nicholas Boaz anatoa tathmini yake kuhusu suala hilo akihojiwa na Babu Abdalla.