Vijana wa kiislamu wahujumu msikiti Burundi:
26 Novemba 2003Matangazo
BUJUMBURA: Watu kadhaa wamejeruhiwa jana, vijana wa kiislamu walipofyetua risasi kwenye msikiti mmoja kaskazini-magharibi mwa Burundi, wakati watu wakisali sala ya IDI-FITR kwa ajili ya kumalizika funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,- kwa mujibu wa shirika la habari la Burundi. Washambuliaji wane wametiwa nguvuni na askari polisi, na wanashikiliwa katika gereza moja la CIBITOKE kaskazini-magharibi mwa Burundi. Vijana hao ni wafuasi wa tawi lililoasi la chama cha waislamu wa Burundi, COMIBU.