1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya usalama vya UN huko DRC kutumia nguvu

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CafB

GOMA.Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa huko Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokasi ya Kongo yamesema kuwa yatatumia nguvu kuwazuia waasi wa Generali Laurent Nkunda kuuteka mji wa Sake.

Waasi hao wametishia kuuteka mji huo wa Sake uliyoko kilomita 30 magharibi mwa Goma ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Vikosi vya waasi hapo juzi viliviteka vijiji viwili muhimu, lakini majeshi ya serikali yamesema kuwa yanajipanga upya kuweza kuvirejesha mikononi mwao vijiji hivyo.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa katika miezi michache iliyopita zaidi ya watu laki nne wamelazimika kuyakimbia makazi yao huko Kivu ya Kaskazini kutokana na kuongezeka kwa mapigano.

Mjini Berlin Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imesema kuwa imeongeza msaada wake kwa wahanga wa mapigano hayo wa euro millioni moja na kufanya msaada uliyotolewa na Ujerumani kufikia euro millioni 4 na 19.