Vilabu vya Ulaya vinataka usawa wa mapato
23 Mei 2016Chama cha Ligi za Kandanda la Kulipwa barani Ulaya – EPFL pia kimesisitiza kuwa kinapinga mapendekezo ya kuundwa kile kinachojulikana kama "Super League" au Ligi Maalum au mfumo wowote ambao unavihakikishia vilabu vikubwa nafasi ya kudumu katika Champions League
Shirikisho la kandanda Ulaya – UEFA hugawa asilimia 75 ya mapato kutoka mashindano yake ya vilabu miongoni mwa vilabu vinavyoshiriki. Karibu nusu ya mapato hayo hutolewa kupitia mfuko wa mauzo, ambayo yanasambazwa kulingana na thamani ya kila soko la matangazo ya televisheni kwa kila nchi. Ina maana kuwa vilabu kutoka baadhi ya nchi hupokea mgwawo mkubwa kabisa kuliko nyingine kwa idadi sawa ya mechi.
EPFL inasema kuwa mfumo wa sasa unapaswa kubakia ambapo vilabu vinavyocheza katika mashindano ya UEFA vinafanya hivyo kwa kufuzu kutoka ligi zao za nyumbani. Wasiwasi unaendelea kuongezeka kuhusu pango baina ya vilabu vichache maarufu na vinginevyo, ambapo Champions League imetawaliwa na idadi ndogo ya vilabu vikubwa.
Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman