1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Viongozi wa ECOWAS wakutana kwenye mkutano wa kilele

15 Desemba 2024

Viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS wakusanyika Abuja kujadilia masuala kadhaa, kubwa likiwa ni usalama na kujiondoa kwa mataifa matatu yanayoongozwa na wanajeshi.

https://p.dw.com/p/4oAQF
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya ECOWAS na Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Nigerian Presidency/Anadolu/picture alliance

Viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS  wamekusanyika leo Jumapili katika mkutano wa kilele.

Burkina Faso, Mali na Niger zimetangaza kuwa uamuzi wao wa kujiondoa haubadiliki, na kuilaumu ECOWAS kwa kuwa kibaraka wa Ufaransa, mtawala wao wa zamani.

Kujiondoa kwa mataifa hayo matatu kunatarajiwa kuwa na athari kubwa kwa biashara huria, usafiri wa watu, na ushirikiano wa kiusalama katika eneo hilo ambako makundi ya wapiganaji wa jihadi yanaendelea kupata nguvu katika kanda ya Sahel.

Mataifa hayo yameunda muungano wao, unaojulikana kama Muungano wa Mataifa ya Sahel, AES, na kuelekeza ushirikiano wao kwa Urusi badala ya Ufaransa. ECOWAS imekabiliana na changamoto za mapinduzi ya kijeshi na mashambulizi ya wapiganaji.