Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameyahimiza mataifa ya umoja huo kuonyesha mshikamano katika kupambana na janga la virusi vya corona na kujenga muungano imara wa afya. Hayo ni miongoni mwa masuala aliyoyazungumza alipolihutubia bunge la Ulaya. Grace Kabogo alizungumza na Abdullah Salim Mzee, mchambuzi wa siasa za kimataifa kuhusu hotuba hiyo.