1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Upinzani Korea Kusini wawasilisha ombi la kumshitaki rais

4 Desemba 2024

Shinikizo linazidi kumuelemea Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol la kumtaka ajiuzulu, baada ya amri ya kijeshi aliyoitangaza jana Jumatatu, wakati vyama vya upinzani vikiwasilisha ombi la kumshitaki kiongozi huyo.

https://p.dw.com/p/4nido
04.12.2024, Südkorea, Seoul: Südkoreaner halten Schilder mit der Aufschrift "Ausweisung von Yoon Suk Yeol" während einer Kundgebung in Seoul, Südkorea
Waandamanaji katika mkusanyiko wa kumtaka Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ajiuzulu Seoul, Korea Kusini, Jumatano, Desemba 4, 2024.Picha: Ahn Young-joon/AP/dpa/picture alliance

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic pamoja na vingine vidogo vitano vimewasilisha ombi hilo alfajiri ya leo, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la Yonhap. Tangazohilo lilisainiwa na wabunge 191, bila ya wabunge wa chama tawala.Wanapanga kuliwasilisha ombi hilo katika vikao vya awali vya bunge hii leo, wakati kura ikitarajiwa kupigwa siku ya Ijumaa ama Jumamosi, limesema shirika hilo la Yonhap.