Waafrika Kusini wachagua wabunge
7 Mei 2014Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa tangu alfajiri saa 11 na vitafungwa rasmi saa 1 usiku ambapo matokeo ya kwanza yataanza kufamika kesho mchana.
Huu ni uchaguzi wa bunge wa kwanza ambapo vijana walozaliwa baada ya kumalizika utawala wa ubaguzi, watashiriki.
Baadhi ya wataalamu wanahisi kwamba shauku na umaarufu uliokuweko wakati wa uhai wa Nelson mandela kwa chama hicho huenda ukapunguwa, huku wapiga kura wakifikiria zaidi juu ya kuzorota kwa hali kiuchumi na visa vilivyoukumba muhula wa kwanza wa rais Jacob Zuma ikiwa ni pamoja na rushwa miongoni mwa vigogo serikalini.
Ni raia milioni 25,3 watakao wachaguwa wabunge 400 ambao ambao hapo mei 21 watamchaguwa rais wa nchi hiyo.
Akiwa na umri wa miaka 72 rais Jacob Zuma atanarajia kuchaguliwa kwa muhla mwingine wa miaka 5.
Uchaguzi wa kutatanisha
Uchaguzi huu umetajwa kama wa " kutatanisha zaidi " katika kipindi cha miaka 20 ya nyuma, alisema Lizette Lancaster mtaalam kwenye taasisi ya utafiti wa usalama. Na kwamba walitarajia " ANC kitapoteza uwanja wake".
Mpinzani mkuu wa chama ANC, muungano wa kidemokrasia Democratic alliance ,ulipata kura 16, 7 katika uchaguzi wa 2009, licha yakusonga mbele tangu wakati huo, lakini kinazingatiwa kama kituvu chake ni chama cha wazungu.
Changamoto nyingine kwa chama ANC, ni kutoka chama cha ukombozi wa kiuchumi EFF kinacho ongozwa na mkuu wa zamani wa tawi la vijana wa ANC Julius Malema, ambaye alifikia hata kuvaa kofia nyekundu akimuigiza rais wa zamani msosialisti wa Venezuela , hayati Hugo Chaves.
Julius Malema na chama chake kipya katika siasa za afrika kusini aweka mbele utaifa, na kuahidi kutaifa sekta kama benkim na madini na kupokonya mali za wazungu wenye kumiliki mashamba makubwa pasina kulipa fidia, na kugawa upya utajiri wa nchi kwa namna iliyo sawa.
Jana Malema aliwahutubia wachimba migodi waliyo mgomoni tangu januari. katika maeneo ya kakszini. " Kama hamtopiga kura chama ANC kitasalia madarakani" Hata kama mko mgomoni lazima kesho mwende kupiga kura hata kama mko mgomoni, hatima ya nchi hii iko mikononi mwenu, alisisitiza kiongozi huyo kijana ".
Hadi kwenye saa za mwisho jana viongozi wa usalama walikuwa wakitowa mwito ya utulivu kwenye siku hii ya uchaguzi, wakati maandamano yenye ghasia yalivikumba vitongoji na mitaa inayo kaliwa na watu wengi masikini hususan Johannesburg.
Afrika kusini imesalia nchi isiyo na usawa licha ya kumalizika utawala wa ubaguzi, ambapo wazungu waanapokea mara 6 zaidi ya raia weusi. Pia hawakabiliwi na ukosefu ajira kama ilivyo kwa weusi na wakipata elimu ambayo weusi hawaipati.
Ikiwa na ukuwaji unao kadiriwa sawa na asilimia 3, 3 katika miaka 20 ya nyuma Afrika kusini bado iko mbali na kutimiza mkakati wa kuwapatia ajira mamilioni ya raia wake wasio na kazi.
Mwandishi/ Amida ISSA
Mhariri / Mohammed Abdul-Rahman
.
.