1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wa habari waachiwa huru nchini Burundi

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdR

Mahakama kuu ya Burundi imewaachia huru waandishi wa habari watatu waliyokuwa wakituhumiwa kuhusika na mpango wa kutaka kuipindua serikali ya nchi hiyo.

Waandishi hao wa habari walikuwa rumande kwa siku kadhaa hadi jana mahakama ilipowaona hawana hatia.Mwendesha mashtaka wa serikali alitaka wafungwe miaka mitatu.

Waandishi hao wa habari walikamatwa Novemba mwaka jana wakituhumiwa kuhusika na mpango wa kutaka kuipundua serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.

Burundi imekumbwa na mapinduzi kadhaa na majaribio ya mapinduzi toka ilipopata uhuru wake kutoka kwa wabeleshi mwaka 1962.Kwa sasa inajaribu kurejea katika hali ya amani baada ya miaka 13 ya vita vya kikabila vilivyopelekea vifo vya zaidi ya watu laki tatu.