Wabunge kutoka shirikisho la mabunge ulimwenguni IPU wanaokutana katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali wamejikuta wakitofautiana misimamo yao kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wakati wakijadili changamoto mbalimbali zinazoendelea ulimwenguni kuhusu masuala ya usalama na unyanyasaji wa kijinsia. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera alituarifu zaidi.