1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafadhili wa kilabu ya Paris waipunguzia mzigo wa madeni Zambia

12 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEF

Wafadhili wa kilabu ya Paris wameamua kuipinguzia madeni yake Zambia.Uamuzi huo umepitishwa kuambatana na utaratibu wa kuzipunguzia madeni nchi masikini kabisa za dunia.Katika mkutano wao mjini Paris,wawakilishi wa nchi fadhili wamekubaliana kufutilia mbali madeni ya Zambia yenye thamani ya dala bilioni moja nukta nne.Mkopo jumla wa Zambia ulikadiriwa kufikia dala bilioni sabaa mwishoni mwa mwaka 2003..Zambia imeahidi kutumia fedha ilizosamehewa kugharimia mikakati muhimu ya kupunguza hali ya umasikini.Mapema wawakilishi wa mataifa fadhili ya kilabu ya Paris,walikubaliana kufuata mia bin mia madeni ya Rwanda.