1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wawili wa UN watekwa nyara DRC

Daniel Gakuba
14 Machi 2017

Msemaji wa serikali Lambert Mende amesema mmarekani Michael Sharp na msweden Zahida Katalan walichukuliwa mateka pamoja na raia wanne wa Kongo.

https://p.dw.com/p/2Z8bB
Inga dams DR Congo Infografik

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha kutekwa nyara kwa wafanyakazi wawili wa Umoja wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kasai katikati mwa nchi hiyo. Msemaji wa serikali Lambert Mende amesema mmarekani Michael Sharp na msweden Zahida Katalan walichukuliwa mateka pamoja na raia wanne wa Kongo; madereva watatu na mkalimani, walipokuwa wakisafiri kwa pikipiki katikati mwa jimbo la Kasai. Haijabainishwa lini utekaji nyara huo ulifanyika, na waliochukuwa watu hao bado hawajatangaza chochote. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, umesema unafanya kila linalowezekana kujua walipo watu hao.