Wafuasi wa Kabila waunda muungano
2 Julai 2018Wapiga kampeni wa kumuunga Rais Kabila, ambaye wakosoaji wanamshutumu kwa kutaka kuwania muhula wa tatu kinyume na sheria, walianzisha kundi hilo siku ya Jumapili (Julai 1) bila ya kusema iwapo atagombea katika uchaguzi huo muhumu mwaka huu.
Hatua hiyo inakuja huku kukiwa na uvumi mkali kuhusiana na iwapo Kabila, ambaye amekuwapo madarakani tangu mwaka 2001, atawania muhula mwingine katika uchaguzi ambao umeahirishwa mara mbili hapo Desemba 23.
Kundi hilo linalojulikana kama Common Front for Congo (FCC), ambalo limemtaja Kabila kuwa mwenye "mamlaka ya kiroho", linataka kukamata madaraka kwa njia ya kidemokrasia kwa kumuunga mkono mgombea pekee katika uchaguzi wa rais kwa misingi ya mpango wa pamoja, kwa mujibu wa mkuu wa ofisi ya rais, Nehemiah Mwilanya Wilondja.
Hata hivyo, Kabila hajaweka wazi nia yake licha ya miito kutoka Marekani, Ufaransa na Uingereza kumtaka atangaze wazi kwamba hatagombea tena.