1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wageni wasioalikwa – Ugonjwa wa Malaria

1 Juni 2011

Ni viumbe wadogo sana, hukuvamia na kukushambulia wakati wa usiku na ni hatari kwa usalama: Hawa ni mbu wanaosababisha ugonjwa wa malaria.Ugonjwa wa malaria ndio hatari zaidi barani Afrika lakini ni rahisi kujikinga nao.

https://p.dw.com/p/McZy
Vinamasi na maziwa ni maeneo yanayopendwa sana na mbu kuzaanaPicha: LAI F

Ugonjwa wa malaria ndio tisho kubwa barani Afrika. Huwaua watu wasiopungua milioni moja kila mwaka kote ulimwenguni. Asilimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na malaria hutokea barani Afrika. Akinamama wajawazito na watoto ndio waliomo hatarini zaidi, na mara nyingi ni watu maskini wanaofariki kutokana na ugonjwa huu kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Na kama tujuavyo, kinga ni bora kuliko tiba. Baadhi ya viini vinavyosababisha ugonjwa huu huwa sugu na haviwezi kutibiwa na aina yoyote ya dawa. Lakini kuna njia rahisi ya kukinga ugonjwa huu. Kwa mfano kutumia vyandarua kukinga mbu au kuvalia mavazi marefu wakati wa usiku.

Lakini kwa mengi zaidi kuhusu mbinu za kukabiliana na ugonjwa wa malaria ungana nasi kwenye mfululizo wa vipindi hivi kuhusu ugonjwa wa malaria wakati tunafunga safari ya kukutana na familia moja barani Afrika katika juhudi yake ya kupambana na malaria.

Vipindi vya “Learning by Ear” Noa bongo Jenga Maisha yako - vinasikika katika lugha sita; Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kireno na Amharic. Vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani