1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGhana

Waghana wapiga kura ya kumchagua Rais na Wabunge

7 Desemba 2024

Raia wa Ghana zaidi ya milioni 18 wameshiriki kwenye zoezi la kupiga kura Jumamosi katika uchaguzi mkuu nchini humo.

https://p.dw.com/p/4nsCh
Ghana I Wahlen
Picha: Julius Mortsi/ZUMAPRESS/picture alliance

Wapiga kura wanamchagua mrithi wa Rais Nana Akufo-Addo, ambaye anaachia ngazi baada ya kuitumikia mihula miwili pia Waghana wanawachagua wawakilishi wa bunge jipya la nchi hiyo.

Kati ya wagombea 11 wanaowania wadhifa wa urais, wagombea wakuu ni makamu wa rais Mahamadu Bawumia, anayekiwakilisha chama tawala cha New Patriotic Party (NPP), na John Dramani Mahama wa chama cha National Democratic Congress (NDC) ambaye alikuwa rais wa nchi hiyo kutoka 2012 hadi mapema 2017.

Nana Akufo-Addo, Rais wa Ghana
Rais wa Ghana anayemaliza muda wake Nana Akufo-AddoPicha: Michael Kappeler/dpa

Matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutangazwa mara baa ya zoezi la uchaguzi kumalizika na kura kuanza kuhesabisa huku matokeo rasmi ya kwanza yakipangiwa kuanza kutolewa siku ya Jumanne.

Soma Pia:  Mahakama ya Ghana yabatilisha uamuzi wa kusitisha shughuli za bunge

Ghana ina historia ya utulivu wa kisiasa, vyama viwili vikuu vya New Patriotic Party (NPP) na cha National Democratic Congress (NDC), vimepishana madarakani kwa amani tangu nchi hiyo iliporejesha demokrasia ya vyama vingi manamo mwaka 1992.

Chama cha NPP kimesema kinatarajia mgombea wake Bawumia atashinda kwenye uchaguzi huo ili kuiongoza nchi kwa mihula miwili ya miaka minne minne madarakani na iwapo kitashinda chama cha NPP kitakuwa madarakani kwa muhula wa tatu madarakani jambo ambalo halijawahi kushuudiwa nchini Ghana.

Ghana I Uchaguzi
Wafuasi wa chama NDC nchini GhanaPicha: Misper Apawu/AP/picture alliance

Makamu wa Rais Muhamadu Bawumia, mwanauchumi aliyepata elimu yake nchini Uingereza na mfanyakazi wa zamani katika benki kuu, ameashiria kuufufua uchumi na kuendeleza mipango endelevu ya serikali ya kuweka mfumo wa kidijitali ili kurahisisha biashara pamoja na kuhakikisha kuwa Ghana inaweka mfumo wa elimu bila malipo na pia kuzipiga tafu programu za afya nchni humo.

Soma Pia: Chama tawala Ghana chamteua mgombea wake wa uchaguzi wa 2024 

Mgombea wa chama cha NDC John Dramani Mahama wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo kutoka 2012 hadi mapema mwaka 2017 amesema mipango yake iwapo atachaguliwa ni kuiweka Ghana katika sura mpya, kuanzisha uchumi wa saa 24, kuongeza muda wa saa za viwandani ili kuongeza nafasi za ajira na uzalishaji zaidi na pia amesema atajadili upya sehemu za mkataba wa shirika la IMF.

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Ghana ambapo ni zaidi ya asilimia 14 na kupanda kwa gharama ya maisha ndio masuala makuu ambayo wananchi wanataka kuona yakipatiwa ufumbuzi na kiongozi mpya atakayechaguliwa.

Ghana I Uchaguzi
Afisa wa polisi akipiga kuraPicha: Julius Mortsi/ZUMAPRESS/picture alliance

Utafiti wa maoni uliofanywa na taasisi ya Afrobarometer, umeonesha kuwa asilimia 82 ya Waghana wanahisi kwamba nchi yao inaelekea upande usiofaa.

Soma Pia: Ghana kuzingatia nidhamu kuhusu mkopo wa IMF

Wizara ya mambo ya ndani imesma serikali ya Ghana imefunga kwa muda mipaka yote ya ardhini tangu Ijumaa usiku hadi Jumapili ili kuhakikisha mchakato wa kura unaendelea vizuri kura, taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ilisema.

Vyanzo:AFP/AP