1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea 26 kuwania urais Kongo

Sekione Kitojo9 Agosti 2018

Wagombea 26 wa urais nchini Kongo wameorodheshwa na tume huru ya uchaguzi. Miongoni mwao wanawake 3 na mawaziri wakuu wazamani 3. Daftari la kudumu la wagombea litatangazwa Septemba 19 kabla ya uchaguzi wa Disemba 23.

https://p.dw.com/p/32scS
Kongo Emmanuel Ramazani Shadary
Picha: REUTERS

Idadi ya wagombea imefikia 26 huku wagombea huru wakiwa 16,na 8 wakiwa wagombea wa vyama vya upinzani.Uchaguzi huo wa duru moja pekee umeorodhesha wagombea mara mbili zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Wagombea hawakujali ati ya ugombeaji ambayo ni dola za kimarekani laki moja na mabazo hazirejeshwi kwa mgombea ikiwa fomu yake itatupiliwa mbali ama kutofauu kweye uchaguzi.

Jumatano pekee ni wagombea 18 waliojiorodhesha akiwemo mgombea alieteuliwa na rais Joseph kabila,Emanuel Shadari. Shadari amesema akichaguliwa atahakikisha kwamba wananchi wanaishi kwa amani na hali yao ya maisha kuboreka.

Ferdinand Kambere ,naibu katibu mtendaji wa chama tawala cha PPRD , amesema kwamba uteuzi wa Shadary ni alama kwamba ni shujaa wa demokrasia nchini.

Demokratische Republik Kongo Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, aliyeamua kutowania tena kiti cha urais.Picha: Getty Images/AFP/T. Nicolon

Kwa upande wake upinzani umelezea kwamba uteuzi wa mgombea wa chama tawala, ni hatua ya ushindi wa demokrasia,lakini wametarajia mageuzi wakati wa uchaguzi. Martin Fayulu ambaye ni mgombea wa vuguvugu Dynamique de l'opposition amesema raia ndie anayetakiwa kuamua kupitia uchaguzi huru.

Amesema hawana maoni yeyote kufuatia uteuzi huo wa mrithi wa Kabila, na kwamba ni mambo yao ya ndani, kwa kuwa Kabila anajua umuhimu wa maamuzi yake. Amesema ikiwa amepanga njama ya kurejea madarakani baadae kama alivyofanya Putin-na Medvedev hilo ni haki yake, lakini akionya kwamba wanachotaka uwepo wa uchaguzi huru, wa wazi na wa kidemokrasia ilikuruhusu raia wa Kongo kujichagulia viongozi wao wenyewe.

Miongoni mwa wagombea 8 wa upinzani ni pamoja na Jeanpierre Bemba, Vital Kamerhe na Felix Tshisekedi kiongozi wa chama cha UDPS. Wagombea watatu ni wanawake ambao wawili wameishi ugenini akiwemo bi Monique Mukuna.

Antoine Gizenga ,mwenye umri wa miaka 94,waziri mkuu wa zamani na pia mshirika wa zamani wa rais Kabila ni mgombea pia wa kiti cha urais. Kuna pia mawaziri wakuu wa zamani 2 Adolphe Muzito na Samy Badibanga ambao ni wagombea pia.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo.

Mhariri: Sekione Kitojo.