MigogoroTunisia
Wahamiaji 27 wapoteza maisha katika bahari ya Mediterenia
2 Januari 2025Matangazo
Boti hizo zilizama katika bahari hiyo nje kidogo ya mji wa Sfax eneo linalotumika na wahamiaji hao kuondoka kuelekea katika mataifa ya Ulaya. Walinzi hao wamesema wamefanikiwa kuwaokoa watu 87 waliokuwa katika boti hizo.
Soma pia: Wahamiaji wengi waliangamia baharini wakienda Uhispania 2024
Mwezi uliopita walinzi wa pwani ya Tunisia waliiopoa pia miili ya wahamiaji wengine 30 katika matukio mawili tofauti baada ya boti zao kuzama wakati walipokuwa wanaelekea Ulaya.
Tunisia inakabiliana na mgogoro wa wakimbizi na imechukua nafasi ya Libya kama eneo linalotumika sana na wahamiaji kutoka Tunisia na maeneo mengine ya Afrika wanaotafuta maisha mazuri Ulaya.