Idadi ya wahamiaji wanaomiminika Ujerumani bado inaongezeka na haitarajiwi kubadilika. Kuna wanaoingia na familia zao na kuna watoto wanaoingia bila ya wazee wao. Sura ya Ujerumani inamulika idadi ya wahamiaji watoto wanaomiminika Ujerumani na namna wanavyoshughulikiwa.