Maelfu ya wanajeshi kutoka afrika Magharibi walipelekwa kupigana vita vya pili vya dunia barani Ulaya kuanzia mwaka 1939 na kuendelea - na hawakulipwa fidia. Idadi kubwa ilitokea katika makoloni ya Uingereza. Katika Makala Yetu Leo, tunaangazia wahanga wa vita vikuu vya pili vya dunia wa Kiafrika waliosahaulika.