Miongoni mwa ambayo yanaangaziwa na wahariri wa Ujerumani wiki hii panapohusika Afrika ni matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo yamempa ushindi Felix Tshisekedi mbele ya mgombea mwengine wa upinzani, Martin Fayulu, na yule wa chama tawala, Emmanuel Shadary.