1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahusika katika Noa Bongo! Jenga maisha yako!

24 Mei 2011

Wanatoka katika maeneo mbali mbali ya Afrika. Ni waandishi wenye uzoefu, waandaaji vipindi vya radio na waandishi wa michezo ya radio. Kutana na baadhi ya wahusika wanaokuletea Learning by Ear - Noa Bongo!

https://p.dw.com/p/EjYQ
Zainab Aziz, mwandishi wa mchezo wa redioPicha: DW

Hope Azeda ni mtaalamu anayechanganya masuala ya burudani na habari. Ni raia wa Rwanda ambaye ameandika na kuelekeza michezo kadhaa ya kuigiza kuhusu masuala muhimu ya kijamii. Mbali na hayo, ni mshauri wa asasi zisizo za kiserikali pamoja na taasisi za serikali.

Ana diploma katika masuala ya muziki, mchezaji ngoma pamoja na tamthilia kutoka chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda.

Justine Bitagoye alianza kazi akiwa kama mwandishi habari na mtangazaji katika televisheni nchini mwake Burundi. Katika tamasha la filamu, Bara la Afrika, FESPACO, alizusha hisia kali kutokana na filamu yake ya maisha halisi, iliyopewa jina la “Mieux vant mal vivre que mourir” ambayo inahusu watoto ambao wanaishi katika mlima wa jaa la taka. Kama alivyo Hope, Justine ana shahada ya uzamili kutoka chuo kikuu cha Makerere mjini Kampala. Katika Learning by Ear - Noa Bongo! anaandika kuhusu athari za utandawazi.

Alex Billy Gitta ni mwandishi habari kijana kutoka Uganda. Anaripoti habari zinazotukia kwa ajili ya kituo cha redio cha KFM 93.3 katika mji mkuu wa Uganda, Kampala. Amejifunza kuwa mwandishi wa habari katika taasisi ya mawasiliano ya umma na alihudhuria mafunzo katika vituo vya utangazaji vya BBC na Deutsche Welle.

Learing by Ear Team Deutsche Welle
Sekretariat ya Noa Bongo-Jenga Maisha Yako iliyoko BonnPicha: DW

Christine Harjes kutoka Ujerumani kila mara alipenda kuondoka kijijini kwake kaskazini mwa Ujerumani kuona mambo mapya duniani. Njiani, alitumbukia katika mapenzi na bara moja mahsusi: Afrika. Amekuwa akiripoti kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na Burkina Faso kwa ajili ya Deutsche Welle. Hivi sasa ni meneja wa mradi wa Learning by Ear - Noa Bongo.

Pierre Kazoni kutoka Burkina Faso ana uchu wa vitu viwili muhimu: Kufundisha na uandishi wa habari. Amefundisha Kiingereza katika shule mbali

mbali nchini Burkina Faso, na wakati huo huo akifanya kazi kama mwandishi habari wa redio ya taifa na televisheni ya Burkina Faso. Ana fahari kujumuisha vipaji hivyo kuweza kutayarisha vipindi vya kuelimisha kwa ajili ya Learning by Ear - Noa Bongo.

Sam Tolulope Olukoya ni mwandishi habari maarufu wa televisheni, redio na magazeti nchini mwake Nigeria. Anaripoti kutoka jiji la Lagos na ametunukiwa tuzo mbalimbali kutokana na ripoti zake za kuvutia: “Ripota wa mwaka wa visa vya uhalifu” na “Ripota wa mwaka wa radio“ ni tuzo mbili tu miongoni mwa nyingine kadhaa alizotunukiwa. Katika kipindi cha Learning by Ear – Noa bongo!, Sam amekutana na baadhi ya vijana wengi mabingwa waliofamikiwa katika fani hii wenye mafanikio. Anataka kuwahimiza vijana wa Afrika kuweza kupata kazi nzuri kwa ajili ya maisha yao.

Zainab Aziz Salim alitoa mkono wa kwaheri kwa nchi yake alikozaliwa, Kenya, lakini hujisikia vizuri anapochangia katika maendeleo ya Afrika kwa kutayarisha riwaya kwa ajili ya Learning by Ear - Noa Bongo. Mwandishi habari wa siku nyingi, akiwa amefanya kazi katika shirika la utangazaji la Kenya, KBC, na pia Deutsche Welle katika idhaa ya Kiswahili. Anapendelea sana vipindi vya kutoa elimu kuhusu HIV na ukimwi, AIDS.