Kutokuwa na uhakika wa nishati ya umeme kwa baadhi ya shule nchini Tanzania hasa zilizo katika maeneo ya vijijini, ni tatizo ambalo limeendelea kuyakumba maeneo mengi na kushusha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi. Sikiliza makala ya Veronica Natalis akionesha juhudi za wanafunzi wa shule ya Sekondari Helene Lange ya Ujerumani waliposaidia shule ya Msitu wa Tembo taa za nishati ya jua.