Gavana wa kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya Anne Waiguru amewataja wakazi wa eneo la mlima Kenya kuwa tayari kumuunga mkono mgombea wa urais kutokea kabila jengine ili kuondoa dhana za utengano. Wakati huohuo, huku kaunti ya Nairobi ikisubiri kuupigia kura mswada wa mageuzi ya katiba wa punguza mzigo, mwasisi wake, amepuuza kauli za wanaodai kuwa naibu wa rais ndiye mfadhili wake.