Wakimbizi waliosahaulika: Warohingya waanzisha makaazi Bangladesh
Zaidi ya Warohingya 70,000 wamekimbia Myanmar na kwenda Bangladesh tangu kuzuka kwa machafuko mwezi Octoba. Takriban nusu ya Milioni ya wakimbizi wako Bangladesh. Wanaishi katika kambi zilizofurika kama ya Kutupalong
Kuikimbia Myanmar
Mnamo mwezi Octoba, kundi la Warohingya lilituhumiwa kwa mauaji ya polisi huko Myanmar. Tangu hapo, kundi hilo la waislamu walio wachache limekuwa likikabiliwa na mashambulizi katika nchi hiyo inayokaliwa na Waislamu wengi wa Kibuddha. Zaidi ya Warohingya 70,000 wamekimbilia Bangladesh. Moja ya kambi wanazoishi iko Kutupalong.
Shughuli za kujitegemea ni muhimu
Warohingya wanaweza kuishi kwa usalama na kuepuka vitisho vya jeshi la Myanmar, ingawa maisha katika kambi hii ya Kutupalong si rahisi hata kidogo. Hakuna miundombinu ya uhakika na wana nyumba za muda tu zilizotengenezwa na wakimbizi wenyewe. Kulingana na mashirika ya haki za binaadamu, walikimbia Myanmar baada ya jeshi kuchoma nyumba zao, kuwabaka na kuuwa mamia ya raia.
Hakuna michezo ya watoto
Hakuna maji yanayotiririka katika maeneo mengi ya kambi hiyo, na kuwawezesha maelfu ya wakimbizi na watoto wao kupata huduma ya maji. Mtoto huyu amebeba udongo alioutoa katika moja ya mto uliopo ndani ya kambi hiyo.
Maisha ya wasiwasi
Udongo na vifaa vingine muhimu hutumika kujengea nyumba katika kambi hiyo ili angalau wakazi hao wapate nyumba iliyofunikwa kwa dari.
Mzozo wa muda mrefu
Huko Myanmar, Warohingya wamekuwa wakitengwa tangu kabla ya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Waingereza mnamo mwaka 1948. Kundi hilo hadi sasa limeendelea kukataliwa kama raia wa Myanmar, pamoja na kupiga kura.
Watafukuzwa tena?
Warohingya pia wameshuhudia kutengwa hata huko Bangladeshi walikokimbilia, ambako serikali imezikatalia boti zilizokuwa na mamia ya wakimbizi kwa madai kwamba tayari makambi yalikuwa yamefurika. Hivi sasa, serikali ya Bangaldesh inapanga kuwahamisha Warohingya na kuwapeleka katika Kisiwa cha mbali ambacho mara nyingi hufunikwa na maji hasa katika majira ya upepo mkali.
Kutengwa katika Kisiwa
Kisiwa cha Thengar Char, ambako serikali ya Bangladesh inataka kuwahamishia Warohingya kiko maili nyingi kutoka bara, na kinafikika kwa njia ya boti tu na kiliwahi kuvamiwa na maharamia wakati fulani huko nyuma. Mratibu wa taasisi isiyo ya serikali inayowasaidia Warohingya aliwahi kuiambia DW kwamba kuna uwezekano finyu wa kutengeneza mkaazi katika Kisiwa hicho cha Thengar Char.
Rekodi mbaya ya ufuatiliaji
Waziri wa masuala ya kigeni wa Bangladesh Abul Hassan Mahmood Ali amekiri kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanyika katika Kisiwa cha Thengar Char. "Shughuli ya kuwahamisha itafanyika mara baada ya kukamilika kwa uendelezwaji wa Kisiwa hicho" alisema. Lakini, hata hivyo serikali bado haijafanya chochote kikubwa kuboresha kambi ya Kutupalong, na wakazi wake wamekuwa wakijishughulikia wao wenyewe.
Kufutwa kwenye historia
Kutokuwepo na eneo salama la nchi yao kunawaacha Warohingya wakiwa hawajui mustakabali wao, wakati ambapo Myanamar ikijitahidi kufuta historia yao. Wizara ya mambo ya tamaduni na dini inataraji kutoa kitabu cha masomo ambacho hakitawataja kwa namna yoyote Warohingya. Mwezi Disemba wizara hiyo ilisema "Ukweli halisi ni kwamba neno 'Rohingya' halikuwahi kutumika wala kuwepo katika historia"