Wakongomani hawamtaki Kabila - Utafiti
25 Oktoba 2016Matangazo
Utafiti huo wa nadra ulifanywa kwa ushirikiano kati ya Kundi la Utafiti Kuhusu Congo katika Chuo Kikuu cha New York, Marekani, na Taasisi ya Uchunguzi wa Maoni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ukiwahusisha mahojiano ya moja kwa moja na watu 7,545 kutoka mikoa 26 ya nchi hiyo kati ya Mei na Septemba.
Asilimia 81 ya waliohojiwa walipinga mabadiliko ya katiba kumruhusu Kabila kugombea muhula wa tatu. Aidha, asilimia 33 walisema wangemchagua gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga Moise Katumbi, huku asilimia 18 wakimuunga mkono kiongozi wa upinzani Etienne Tschisekedi.
Ni asilimia 7.8 tu waliosema wangependa kumchagua tena Rais Kabila.