1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakulima kuandamana dhidi ya rais Macron

Josephat Charo
24 Februari 2024

Wakulima wanatarajiwa kuandamana kuonyesha upinzani wao kwa rais Emmanuel Macron mjini Paris kwenye maonyesho makubwa ya kilimo.

https://p.dw.com/p/4cpH3
Polen Bauernproteste | Anti EU
Wakulima wanapinga mkataba wa kuyalinda mazingira unaowabana katika baadhi ya shughuli zao za kilimo na bidhaa za bei nafuu kutoka Ukraine.Picha: Krzysztof Zatycki/ZUMA/picture alliance

Wakulima wanajiandaa kuandama leo dhidi ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati atakapoyatembelea maonesho makubwa ya kilimo mjini Paris, huku kukiwa na ghadhabu kuhusu gharama na sheria za kuyalinda mazingira.

Wakulima wamekuwa wakiandamana kote barani Ulaya wakitaka mapato bora na urasimu upunguzwe na wanalalamika kuhusu ushindani usio wa haki kutoka kwa bidhaa za bei nafuu kutoka nchini Ukraine.

Mwaka 2022 Umoja wa Ulaya uliondoa ushuru wa uagizaji wa chakula kutoka Ukraine kuisaidia nchi hiyo kiuchumi kufuatia uvamizi wa Urusi. Maonesho ya kilimo ya mjini Paris ni tukio kubwa nchini Ufaransa linalowavutia wageni takriban 600,000 katika kipindi cha siku tisa.