1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wales kidedea yatinga nusu fainali

Admin.WagnerD2 Julai 2016

Katika usiku wa kukumbukwa sana katika historia ya kandanda, Wales iliitupa kando Ubelgiji iliyoko nafasi ya pili katika orodha ya timu bora duniani katika mashindano ya Ulaya, Euro 2016 Ijumaa na kutinga nusu fainali.

https://p.dw.com/p/1JHpT
Frankreich Euro 2016 Wales - Belgien Tor Jubel
Wachezaji wa Wales wakishangiria bao la pili dhidi ya Ubelgiji wakiongozwa na Robson-KanuPicha: Reuters/C. Recine

Wales ilivurumuka kutoka mwanzo ambao haukuwa tulivu kwake na kuikandika Ubelgiji mabao 3-1 katika pambano lililojaa heka heka nyingi la robo fainali, kwa magoli yaliyofungwa na washambuliaji wawili ambao hawafahamiki sana.

Kama kawaida , Gareth Bale alikuwa katika hali nzuri kabisa, na mazungumzo kwa kweli yatatuwama kwake na Cristiano Ronaldo wa Ureno wakati timu hizo zitakapokutana katika mpambano wa nusu fainali wiki ijayo.

Frankreich Euro 2016 Wales gegen Belgien Tor Jubel
Nahodha wa Wales Ashley Williams akishangiria bao lake la kusawazishaPicha: Reuters/C. Recine

Wachezaji wawili wenye uzoefu mkubwa katika historia ya kandanda. Wachezaji wanaocheza katika timu moja Real Madrid. Nyota waliomo katika timu mbili zenye mafanikio makubwa katika Euro 2016.

Pamoja na hayo , tofauti na Ureno, Wales pamoja na Bale wamecheza vizuri sana na kwa kweli ni mshangao wa kuburudisha wakati wakifikia awamu ya nusu fainali kwa mara ya kwanza katika mashindano makubwa.

"Tumefurahishwa mno kufikia hapa. Hatujawahi kufika katika kiwango hiki," amesema kocha wa Wales Chris Coleman, ambaye aliichukua timu hiyo ikiwa nje ya timu 100 za juu duniani miaka minne iliyopita. "Unaota kuhusu usiku kama huu. Hufahamu iwapo utakuwa na bahati ya kutosha kushuhudia hiki, na wakati unakuwamo katika mafanikio kama haya , huwezi kusimulia hisia zake.

Frankreich Euro 2016 Wales - Belgien Enttäuschung
Akiwa amekata tamaa Axel Witsel wa UbelgijiPicha: Reuters/J. Sibley

Baada ya dakika 25 jana Ijumaa, ndoto ilionekana kuwa mbali kwa Wales dhidi ya Ubelgiji iliyojichomoza na kuanza kwa kasi , kikosi ambacho kilikuwa kinacheza karibu kama nyumbani kwake kiasi ya kilometa 10 tu kutoka mpaka wake na Ufaransa.

Wachezaji wenye uzoefu

Lakini Ubelgiji ilitanabahi kwamba kutokuwa na wachezaji wawili walinzi wenye uzoefu mkubwa haitakuwa rahisi katika mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Wales.

Hata hivyo , haukuwa rahisi kabisa jana Ijumaa.

Katika mchezo ambao ulionesha udhaifu katika safu yake ya ulinzi, Ubelgiji ilitumbukia katika kipigo cha mabao 3-1, na kwa hiyo nafasi ya kufikia nusu fainali kwa mara ya kwanza katika mashindano makubwa kama haya tangu fainali za kombe la dunia mwaka 1986 iliota mbawa.

Frankreich Euro 2016 Wales gegen Belgien Tor Jubel
Wachezaji wa Ubelgiji wakishangiria bao lao la kuongozaPicha: Reuters/D. Staples

Majeruhi wa Ubelgiji

Kocha Marc Wilmots aliingia katika michuano ya Euro 2016 bila ya wachezaji wa kawaida Vincent Kompany na Nicolas Lombaerts. Kwa mchezo na Wales pia alimkosa Thomas Vermaelen , ambaye alikuwa na kadi mbili za njano na kwa hiyo hakustahili kucheza.

Na kana kwamba mambo hayajakuwa mabaya zaidi, Wilmots alilazimika kumtoa kikosini mlinzi mwenye uzoefu mkubwa wakati Jan Vertonghen alipoumia misuli ya paja wakati wa mazowezi ya mwisho kabla ya kukabiliana na Wales jana.

Frankreich Euro 2016 Wales gegen Belgien Zweikampf
Mpambano kati ya Eden Hazard wa Ubelgiji na Joel Allen wa Wales (kushoto)Picha: Reuters/C. Recine

Waliochukua nafasi zao ! Jason Denayer na Jordan Lukaku, wote wakiwa na umri wa miaka 21, na wakicheza kwa mara ya nane na mwenzake mara ya tano katika kikosi hicho.

"Huwezi kubadilisha uzoefu. Mimi ndio nahusika na hatuwezi kuwalaumu wachezaji vijana," Wilmots amesema. "Unahitaji mashine iliyotiwa mafuta vizuri kuweza kushinda. Tulifanya makosa ambayo hatukupaswa kufanya."

Ni kweli kwamba Ubelgiji ilifanya makosa . Baada ya dakika 20 za kwanza za kucheza kwa nguvu na kustahili kupata bao la kuongoza lililopachikwa wavuni na Radja Nainggolan kwa mkwaju wa mita 25, safu ya kiungo ilianza kupoteza mwelekeo na kurudi nyuma na mbinyo kwa wachezaji wachanga ulionekana dhahiri kuwa mzito.

Fußball UEFA EURO 2016 Deutschland PK Joachim Löw und Mesut Oezil
Katika mkutano na waandishi habari kocha wa Die Mannschaft Joachim LoewPicha: picture-alliance/dpa/UEFA

Mashindano hayo yanaendelea leo ambapo Ujerumani Die Mannschaft , inaoneshana kazi na Squadra Azzurri , timu ya taifa ya Italia. Na jumapili ni zamu ya wenyeji wa mashindano Ufaransa , Le Bleau ikitiana kifuani na timu iliyowashangaza wengi Iceland.