Kufuatia umasikini,ukosefu wa ajira na vita watoto nchini Kongo na hasa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini waamua kujiunga kwa hiari na makundi ya waasi. Hayo yameelezwa na shirika la kimataifa linalopambana kuzuia watoto kuingizwa vitani. Awali watoto wa DRC walikuwa wakiingizwa kwa lazima katika makundi hayo ya waasi.