Wanafunzi wa lugha ya Kijerumani kutoka Burundi kuzuru Ujerumani
18 Juni 2010Matangazo
Kutokana na mpango wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani wa kuanzisha ushirikiano na shule zaidi ya elfu kote ulimwenguni, taasisi ya utamaduni ya Ujerumani, Goethe, tayari imeanzisha ushirikiano na shule moja nchini Burundi.
Wanafunzi 40 wa shule hiyo wamekuwa wakifunzwa lugha ya Kijerumani kwa mara ya kwanza nchini humo. Wanafunzi saba kati yao wamepita mtihani na kuruhusiwa kusafiri kuja hapa Ujerumani mwezi ujao kupata kozi ya wiki 3 katika kuimarisha uwezo wao wa kuzungumza lugha ya Kijerumani.
Mwandhishi wetu kutoka Burundi, Hamida Issa, ametutumia taarifa ifuatayo.
Mwandishi, Hamida Issa
Mpitiaji, Peter Moss
Mhariri, Othman Miraji